Raja Casablanca yaingia katika mgogoro mkubwa, Nabi aondoka Casablanca

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
30 Aug 2026
Raja Casablanca yaingia katika mgogoro mkubwa, Nabi aondoka Casablanca

Raja Casablanca imeingia kwenye sintofahamu baada ya Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Nasreddine Nabi, kuondoka jijini Casablanca na kuelekea Brussels, huku taarifa zikieleza kuwa kuna mvutano ndani ya uongozi wa klabu hiyo.

Chanzo kikuu cha mvutano huo kinatajwa kuwa tofauti za kiutendaji kati ya Nabi na Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, hasa kuhusu masuala ya usajili. Nabi alitarajiwa kuwa na ushawishi katika maamuzi ya usajili baada ya kuteuliwa kuwa kocha, lakini inadaiwa mkurugenzi huyo amekuwa akitaka kuwa na udhibiti mkubwa katika mchakato huo.

Miongoni mwa matukio yaliyoongeza mvutano ni suala la usajili wa Maseko, ambaye Nabi alidaiwa kuwasiliana naye akiwa bado Mamelodi Sundowns na kufikia makubaliano ya awali. Hata hivyo, mpango huo baadaye ulipingwa na Mkurugenzi wa Michezo, jambo lililomfanya Nabi kutoridhishwa na mwenendo wa klabu.

Taarifa hizo pia zinadai kuwa Mkurugenzi wa Michezo huyo alikuwa ameanza mazungumzo na kocha mwingine takribani wiki tatu zilizopita, wakati Nabi bado akiwa kazini. Hali hiyo imeongeza maswali kuhusu mustakabali wa Nabi na namna klabu hiyo inavyoendeshwa, huku mashabiki wakisubiri hatua itakayofuata kutoka kwa uongozi wa Raja Casablanca.

ADVERTISE HERE

More Stories

Pep Guardiola arejea Etihad, Man city ikipigwa 4-2 na PSG
Pep Guardiola arejea Etihad, Man city ikipigwa 4-2 na PSG
3m ago
READ MORE β†’
CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027
Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027
3h ago
READ MORE β†’
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
6h ago
READ MORE β†’
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
13h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
1d ago
READ MORE β†’
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
1d ago
READ MORE β†’
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
1d ago
READ MORE β†’
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
1d ago
READ MORE β†’