Malick Yalcouyé, kutoka ASEC hadi kuwang’ara Brighton na kuacha majuto Simba.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
•
31 Aug 2026
Malick Yalcouyé, kutoka ASEC hadi kuwang’ara Brighton na kuacha majuto Simba.

Malick Yalcouyé ameibuka kuwa miongoni mwa majina yaliyozungumziwa zaidi baada ya kufunga bao katika mchezo wa Brighton dhidi ya Chelsea, huku kiwango chake uwanjani kikifanya mashabiki wengi kuvutiwa na kipaji chake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo, akifunga bao moja, akipiga mashuti mawili yaliyolenga lango, kushinda asilimia 77.8 ya mipambano yake na kukamilisha asilimia 80 ya majaribio yake ya kuwapita wapinzani.

Baada ya muonekano wake kuibua mijadala mitandaoni na baadhi ya watu kuanza kuhoji umri wake, ASEC Mimosas ya Ivory Coast imeamua kuweka wazi historia yake. Klabu hiyo imechapisha picha za Yalcouyé tangu akiwa kwenye akademi yake akiwa mdogo, kwa lengo la kuthibitisha kuwa taarifa zinazohusu umri wake si za kweli. Yalcouyé pia ana tatizo la chronic alopecia, hali inayoweza kusababisha mtu kupoteza nywele akiwa katika umri mdogo, jambo ambalo limechangia baadhi ya watu kushangazwa na muonekano wake.

Kinachofanya simulizi la Yalcouyé livutie zaidi upande wa Tanzania ni kwamba kabla ya kuendelea na safari yake ya soka hadi Ulaya, alihusishwa na Simba SC. Taarifa zinaeleza kuwa mwaka 2022 Simba iliwahi kutuma ofa kwa ajili ya kumsajili Yalcouyé alipokuwa ASEC Mimosas, lakini dili hilo halikukamilika. Inadaiwa ASEC ilikuwa imewataka Simba kulipa ada ya usajili ya takribani dola 250 pekee, lakini Simba ikaamua kutokamilisha uhamisho huo. Miaka kadhaa baadaye, Yalcouyé sasa anaonekana kwenye jukwaa kubwa la soka akiwa Brighton, jambo ambalo linazua swali la kama Simba ilipoteza moja ya fursa adimu ya kugundua kipaji mapema.

Kwa takwimu alizoonyesha dhidi ya Chelsea, Yalcouyé alionyesha kuwa si mchezaji wa kufunga tu bali pia ana uwezo mkubwa wa kushindana na wapinzani, kuwapita na kushiriki katika ujenzi wa mchezo. Alifanya touches 47 na recoveries mbili, huku bao lake likimpa umaarufu zaidi. Brighton tayari imejijengea sifa ya kugundua na kuendeleza vipaji, hivyo kama Yalcouyé ataendelea na kiwango hiki, si jambo la kushangaza kuona thamani yake ikipanda kwa kasi katika miaka ijayo. Kutoka kwenye akademi ya ASEC, kupita kwenye rada ya Simba, hadi kuangaza Premier League, safari ya kijana huyu bado ndiyo inaanza.

ADVERTISE HERE

More Stories

15 de Agosto wawawekea ngumu mashabiki wa Simba
15 de Agosto wawawekea ngumu mashabiki wa Simba
2h ago
READ MORE →
Barcelona yatambulisha jezi ya El Clasico yenye nembo ya Golf Wang
Barcelona yatambulisha jezi ya El Clasico yenye nembo ya Golf Wang
6h ago
READ MORE →
Yanga yaongeza kasi ya maandalizi kuivaa CFFA ya Madagascar
Yanga yaongeza kasi ya maandalizi kuivaa CFFA ya Madagascar
7h ago
READ MORE →
Yanga SC kukamilisha malipo ya Sure Boy ndani ya miezi miwili
Yanga SC kukamilisha malipo ya Sure Boy ndani ya miezi miwili
7h ago
READ MORE →
Pep Guardiola arejea Etihad, Man city ikipigwa 4-2 na PSG
Pep Guardiola arejea Etihad, Man city ikipigwa 4-2 na PSG
7h ago
READ MORE →
CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
CAF yawateua waamuzi wanne wa Tanzania kuchezesha mchezo wa CAFCL
10h ago
READ MORE →
Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027
Sarafu yaamua hatima ya Serengeti Boys, yakosa nafasi AFCON U17 2027
11h ago
READ MORE →
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
Vinicius Junior afungiwa mechi nne, kuukosa mchezo wa El Clasico
14h ago
READ MORE →
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.
20h ago
READ MORE →
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
1d ago
READ MORE →