Ibrahim Doumbia aguswa na mapenzi ya mashabiki wa Simba, hadi machozi yamtoka.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
1 Sep 2026
Ibrahim Doumbia aguswa na mapenzi ya mashabiki wa Simba, hadi machozi yamtoka.

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia, ameguswa kwa kiasi kikubwa na upendo na sapoti aliyopewa na mashabiki wa klabu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Geita Gold.

Doumbia amesema aliposhuka kwenye basi baada ya mchezo huo, aliona bango lililoandikwa “TUKO PAMOJA DOUMBIA, TUNAKUPENDA”, jambo ambalo lilimgusa sana moyoni na kumfanya machozi yamtoke.

Mshambuliaji huyo ameeleza kuwa ujumbe huo kutoka kwa mashabiki umempa nguvu na kumfanya ajione kuwa yupo sehemu ambayo anaaminiwa na kuthaminiwa na familia ya Simba.

Amesema anawashukuru kwa dhati mashabiki wa Simba pamoja na familia nzima ya klabu kwa sapoti, upendo na imani wanayoendelea kumpa, akiahidi kutorudisha nyuma jitihada zake.

Doumbia ameweka wazi kuwa ataendelea kupambana, kufanya kazi kwa bidii na kutoa kila alichonacho kila anapovaa jezi ya Simba, akiamini kuwa juhudi hizo zitasaidia kufikia malengo ya klabu.

Upendo ulioonyeshwa na mashabiki baada ya mchezo huo unaonekana kuwa ishara ya uhusiano mkubwa uliopo kati yao na mchezaji huyo, huku Doumbia akiahidi kuwalipa kwa matokeo na kujituma zaidi uwanjani.

ADVERTISE HERE

More Stories

Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
1h ago
READ MORE β†’
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
1h ago
READ MORE β†’
Kane kuongeza mkataba Bayern Munich hadi 2029
Kane kuongeza mkataba Bayern Munich hadi 2029
2h ago
READ MORE β†’
Reece James afanyiwa upasuaji wa goti
Reece James afanyiwa upasuaji wa goti
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate kurudi Tanzanite Kwaraa, Polisi Tanzania kurejea Ushirika
Fountain Gate kurudi Tanzanite Kwaraa, Polisi Tanzania kurejea Ushirika
6h ago
READ MORE β†’
Beno Kakolanya afunguka sakata la madai ya wachezaji Yanga
Beno Kakolanya afunguka sakata la madai ya wachezaji Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc dimbani Misri kusaka tiketi ya makundi CAFCC
Azam Fc dimbani Misri kusaka tiketi ya makundi CAFCC
7h ago
READ MORE β†’
Didier Drogba kutua Tanzania kuelekea maandalizi ya AFCON 2027
Didier Drogba kutua Tanzania kuelekea maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’