CAF: Timu mwenyeji ndiye mwenye jukumu la urushaji wa matangazo ya mechi hatua za awali

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
2 Sep 2026
CAF: Timu mwenyeji ndiye mwenye jukumu la urushaji wa matangazo ya mechi hatua za awali

Mashabiki wa CAF Champions League na CAF Confederation Cup wameelekezwa kufahamu kuwa katika duru za awali za mashindano hayo, urushaji wa moja kwa moja wa mechi hauko chini ya usimamizi wa CAF, bali jukumu hilo linabebwa na timu mwenyeji.

Kwa mujibu wa utaratibu huo, timu mwenyeji inawajibika kufanya makubaliano na kituo cha televisheni au mtangazaji kwa ajili ya kurusha mchezo. Hivyo, baadhi ya mechi zinaweza kuonyeshwa moja kwa moja huku nyingine zikikumbwa na changamoto za kutorushwa au ubora wa picha na mtandao.

Wadau wa soka wamewataka mashabiki kuelewa hali hiyo, hususani kuelekea mechi za wikendi hii, kwa kuwa endapo mchezo wa klabu yao hautarushwa moja kwa moja au ukawa na changamoto za ubora wa matangazo, suala hilo linapaswa kuhusishwa na timu mwenyeji katika hatua hiyo ya mashindano.

Hata hivyo, kuanzia hatua ya makundi na hatua zinazofuata, CAF itakuwa na jukumu la kusimamia urushaji wa mechi, hatua inayolenga kuweka mfumo mmoja wa matangazo na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza katika duru za awali.

ADVERTISE HERE

More Stories

Yanga yamtumia Mshery langoni dhidi ya CFFA FC, Diarra akosekana
Yanga yamtumia Mshery langoni dhidi ya CFFA FC, Diarra akosekana
1h ago
READ MORE β†’
Ghana yateua benchi la muda kuelekea mchezo dhidi ya Somalia
Ghana yateua benchi la muda kuelekea mchezo dhidi ya Somalia
1h ago
READ MORE β†’
Viwanja vya Afrika kuwaka moto leo katika kombe la shirikisho
Viwanja vya Afrika kuwaka moto leo katika kombe la shirikisho
2h ago
READ MORE β†’
EPL: Mechi tano za kibabe kuchezwa leo
EPL: Mechi tano za kibabe kuchezwa leo
2h ago
READ MORE β†’
Yanga kuendeleza safari ya CAF Champions League dhidi ya CFFA
Yanga kuendeleza safari ya CAF Champions League dhidi ya CFFA
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaondoka na sare dhidi ya ZED FC nchini Misri
Azam FC yaondoka na sare dhidi ya ZED FC nchini Misri
17h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
Ally Kamwe aeleza kuhusu hali ya goli kipa Diarra kuelekea CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
Ally Kamwe afunguka maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya CFFA FC
22h ago
READ MORE β†’
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
Infantino aomba radhi kwa utata wa haki za kibiashara FIFA
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
Yanga yasaka rekodi ya kibabe ligi ya mabingwa
23h ago
READ MORE β†’