CAF yakagua arusha kujiweka tayari kwa afcon 2027.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 4th September 2026

CAF yakagua arusha kujiweka tayari kwa afcon 2027.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya ukaguzi wa miundombinu mbalimbali jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuelekea fainali za AFCON 2027, ambazo Tanzania itaziandaa kwa pamoja na Kenya na Uganda.

Katika ukaguzi huo, CAF imepitia Uwanja wa Arusha, viwanja vya mazoezi pamoja na vituo muhimu vya huduma za afya na matibabu vinavyotarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Ukaguzi huo unaendelea kuonyesha hatua zinazochukuliwa na Tanzania kuhakikisha miundombinu na huduma muhimu zinakidhi viwango vinavyohitajika na CAF kabla ya michuano hiyo kufanyika mwaka 2027.

Tanzania, kupitia ushirikiano wa pamoja na Kenya na Uganda, inaendelea na maandalizi ya kihistoria ya AFCON 2027, huku Arusha ikiwa miongoni mwa maeneo muhimu yanayotarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi na utekelezaji wa mashindano hayo.

More Stories

Massanza akumbana na fainali kamati ya saa 72
Massanza akumbana na fainali kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Kangwanda: Tumejiandaa vizuri, tutatoa kila kitu uwanjani.
Kangwanda: Tumejiandaa vizuri, tutatoa kila kitu uwanjani.
Today, READ MORE β†’
Bodi ya ligi tanzania bara yafuta kadi nyekundu ya Gibril sillah wa Azam
Bodi ya ligi tanzania bara yafuta kadi nyekundu ya Gibril sillah wa Azam
Today, READ MORE β†’
Mngqithi: Gaborone United ni timu imara, Yanga inakabiliwa na mtihani mgumu.
Mngqithi: Gaborone United ni timu imara, Yanga inakabiliwa na mtihani mgumu.
Today, READ MORE β†’
Ahmed Ally atuma ujumbe mzito kwa wachezaji wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya Mighty wanderers
Ahmed Ally atuma ujumbe mzito kwa wachezaji wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya Mighty wanderers
Today, READ MORE β†’
Aziz KI apewa mazoezi ya ziada kuingamiza Gaborone united kesho
Aziz KI apewa mazoezi ya ziada kuingamiza Gaborone united kesho
Today, READ MORE β†’
Bernard Kamungo ajumuishwa rasmi kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Bernard Kamungo ajumuishwa rasmi kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Today, READ MORE β†’
Kikosi Cha awali Taifa Stars hadharani kufuzu Afcon 2027
Kikosi Cha awali Taifa Stars hadharani kufuzu Afcon 2027
Today, READ MORE β†’
CAF yakagua arusha kujiweka tayari kwa afcon 2027.
CAF yakagua arusha kujiweka tayari kwa afcon 2027.
Today, READ MORE β†’
Rushine aahidi makubwa kimataifa, Simba ikielekea malawi
Rushine aahidi makubwa kimataifa, Simba ikielekea malawi
Today, READ MORE β†’