Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz Ki, ameonekana kufanya mazoezi ya ziada baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo nchini Botswana, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.
Hatua hiyo inakuja baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, kueleza kuwa Aziz Ki bado hajafikia kiwango anachokihitaji kutokana na kukosa maandalizi ya msimu (pre-season), jambo linalomfanya mchezaji huyo kuendelea kuongeza juhudi katika maandalizi yake.
Yanga itashuka uwanjani kesho dhidi ya Gaborone United katika mchezo wa mkondo wa kwanza, utakaochezwa nchini Botswana majira ya saa 2 usiku, kabla ya timu hizo kukutana tena katika mchezo wa marudiano Septemba 12, 2026.



