Real Madrid na PSG zakutana na vipigo katika ligi zao.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 5th September 2026

Real Madrid na PSG zakutana na vipigo katika ligi zao.

Real Madrid imeanza kukutana na changamoto katika La Liga baada ya kukubali kichapo cha 1-0 dhidi ya Real Betis katika mchezo wa ugenini. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Parrot dakika ya 81, na kuifanya Betis kuibuka na ushindi muhimu mbele ya mashabiki wake.

Real Madrid ilijaribu kutafuta bao la kusawazisha katika dakika za mwisho, lakini haikuweza kuvunja ulinzi wa Real Betis. Matokeo hayo yanaifanya Madrid kuondoka ugenini bila pointi, huku Betis ikivuna ushindi baada ya kupata bao lake katika kipindi cha mwisho cha mchezo.

Wakati huo huo, Paris Saint-Germain imeendelea kupata matokeo yasiyoridhisha baada ya kupoteza nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya AS Monaco. PSG ilipata bao lake kupitia Marquinhos, lakini Monaco iligeuza mchezo na kupata ushindi kupitia Nazinho dakika ya 58 na Idumbo dakika ya 72.Vipigo hivyo vimekuwa habari kubwa katika soka la Ulaya, huku Real Madrid na PSG zikiwa miongoni mwa timu zinazotarajiwa kufanya vizuri katika msimu huu. Kwa Madrid, kichapo dhidi ya Betis ni pigo katika harakati zake za kuendelea na mwendo mzuri katika La Liga, wakati PSG ikitakiwa kurekebisha mapungufu yake baada ya kupoteza dhidi ya Monaco.

More Stories

Real Madrid na PSG zakutana na vipigo katika ligi zao.
Real Madrid na PSG zakutana na vipigo katika ligi zao.
Today, READ MORE β†’
Chama: Ilikuwa ngumu kucheza dhidi ya simba nikiwa na jezi ya timu nyingine
Chama: Ilikuwa ngumu kucheza dhidi ya simba nikiwa na jezi ya timu nyingine
Today, READ MORE β†’
Clatous Chama : Nilijutia kuondoka simba
Clatous Chama : Nilijutia kuondoka simba
Today, READ MORE β†’
Massanza akumbana na fainali kamati ya saa 72
Massanza akumbana na fainali kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Kangwanda: Tumejiandaa vizuri, tutatoa kila kitu uwanjani.
Kangwanda: Tumejiandaa vizuri, tutatoa kila kitu uwanjani.
Today, READ MORE β†’
Bodi ya ligi tanzania bara yafuta kadi nyekundu ya Gibril sillah wa Azam
Bodi ya ligi tanzania bara yafuta kadi nyekundu ya Gibril sillah wa Azam
Today, READ MORE β†’
Mngqithi: Gaborone United ni timu imara, Yanga inakabiliwa na mtihani mgumu.
Mngqithi: Gaborone United ni timu imara, Yanga inakabiliwa na mtihani mgumu.
Today, READ MORE β†’
Ahmed Ally atuma ujumbe mzito kwa wachezaji wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya Mighty wanderers
Ahmed Ally atuma ujumbe mzito kwa wachezaji wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya Mighty wanderers
Today, READ MORE β†’
Aziz KI apewa mazoezi ya ziada kuingamiza Gaborone united kesho
Aziz KI apewa mazoezi ya ziada kuingamiza Gaborone united kesho
Today, READ MORE β†’
Bernard Kamungo ajumuishwa rasmi kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Bernard Kamungo ajumuishwa rasmi kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Today, READ MORE β†’