Nyota wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, ameitakia kila la kheri timu yake kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana, akieleza kuwa moyo na fikra zake zipo pamoja na kikosi hicho licha ya kutokuwepo uwanjani kutokana na jeraha.
Kupitia ujumbe wake, Zouzoua amesema: βKila la kheri familia nzima ya Yanga kwenye safari ya Ligi ya Mabingwa. Isivyo bahati kutokuwepo kwangu kunanizuia mimi kuwa nanyi dimbani, lakini moyo wangu na fikra zipo pamoja nanyi.β
Zouzoua anatarajiwa kukosa msimu mzima wa 2026/27 baada ya kupata jeraha kubwa la mguu na kifundo cha mguu katika mchezo wa mwisho wa msimu uliopita dhidi ya JKT Tanzania.
Licha ya kutokuwepo kwenye kikosi, Zouzoua amewataka wachezaji wenzake kujitoa kwa kila hali katika kuipambania jezi ya Yanga, huku akisisitiza kuwa ataendelea kuwa pamoja nao kwa moyo katika safari yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika.