Local, Normal News, CAFCC, Singida BS

Singida BS yaweka rekodi Afrika, yagawa dozi nene Sudan Kusini

Joel JJ By Joel JJ
2h ago
Singida BS yaweka rekodi Afrika, yagawa dozi nene Sudan Kusini

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC), timu ya Singida Black Stars, wameweka rekodi Afrika baada ya kupata ushindi mnono na wa kihistoria wa mabao 7-1 ugenini dhidi ya Al Ghazala SC Wau ya nchini Sudan Kusini.

Katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya awali uliopigwa jana Septemba 6, 2026, Singida Black Stars walionyesha kiwango cha hali ya juu na kutawala mchezo huo kuanzia dakika ya kwanza hadi kumpiga mpinzani wake mweleka mzito nyumbani kwake.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa mshambuliaji, Mathew Tegisi, aliyeweka rekodi ya kufunga 'hat-trick' ya mapema ndani ya kipindi cha kwanza.

Tegisi alifungua akaunti ya mabao katika dakika ya 20, kabla ya kuongeza mabao mengine mtawalia katika dakika za 23 na 32.

Kiungo mshambuliaji, Sheikhan Ibrahim, alihitimisha karamu ya mabao ya kipindi cha kwanza kwa kufunga bao la nne katika dakika ya 41, na kupeleka timu hizo mapumziko huku Singida wakiwa mbele kwa mabao 4-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji Al Ghazala wakijaribu kufanya mabadiliko yaliyowasaidia kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Mohammed Zakariya katika dakika ya 70.

Hata hivyo, bao hilo halikuwakatisha tamaa miamba hiyo ya Singida kwani walirudi mchezoni na kupachika mabao mengine kupitia kwa Jonathan Sowah aliyefunga katika dakika za 63 na 90, huku Henry David akipachika bao lingine katika dakika ya 86 na kukamilisha idadi ya mabao saba.

Ushindi huo wa mabao 7-1 unaiweka Singida Black Stars katika nafasi nzuri ya kutinga hatua inayofuata, huku mchezo wa marudiano ukitazamiwa kupigwa nchini Tanzania kati ya Septemba 11 na 13, 2026.

Kama Singida BS itafanikiwa kusonga mbele, itakutana na mshindi kati ya Al Ahli Madani ya Sudan na Tusker FC ya Kenya katika raundi ya pili ya hatua ya kufuzu makundi.

More Stories

Kamwe atangaza sele day kuingamiza Gaborone, mashabiki yanga watakiwa kuiga style yake
Kamwe atangaza sele day kuingamiza Gaborone, mashabiki yanga watakiwa kuiga style yake
45m ago
READ MORE →
Yanga inazidi kuimarika na tunataka ubingwa wa afrika : Manqoba
Yanga inazidi kuimarika na tunataka ubingwa wa afrika : Manqoba
56m ago
READ MORE →
EPL Updates: Everton na Arsenal Zang’ara Katika Michezo ya Leo.
EPL Updates: Everton na Arsenal Zang’ara Katika Michezo ya Leo.
11h ago
READ MORE →
Simba yaunguruma Malawi, yaichapa Mighty Wonderers
Simba yaunguruma Malawi, yaichapa Mighty Wonderers
15h ago
READ MORE →
Highlights : Mighty Wonderers 0-1 Simba
Highlights : Mighty Wonderers 0-1 Simba
16h ago
READ MORE →
Simba kuikabili Mighty wanderers bila Libasse Gueye
Simba kuikabili Mighty wanderers bila Libasse Gueye
23h ago
READ MORE →
Sele Gomez avuruga sherehe Gaborone United dakika za Jioni
Sele Gomez avuruga sherehe Gaborone United dakika za Jioni
1d ago
READ MORE →
Highlights : Gaborone United 1-1 Yanga
Highlights : Gaborone United 1-1 Yanga
1d ago
READ MORE →
Pacome atuma salamu Yanga kuelekea mchezo wa Gaborone united
Pacome atuma salamu Yanga kuelekea mchezo wa Gaborone united
1d ago
READ MORE →