Singida BS yaweka rekodi Afrika, yagawa dozi nene Sudan Kusini

Joel JJ By Joel JJ
•
7 Sep 2026
Singida BS yaweka rekodi Afrika, yagawa dozi nene Sudan Kusini

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC), timu ya Singida Black Stars, wameweka rekodi Afrika baada ya kupata ushindi mnono na wa kihistoria wa mabao 7-1 ugenini dhidi ya Al Ghazala SC Wau ya nchini Sudan Kusini.

Katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya awali uliopigwa jana Septemba 6, 2026, Singida Black Stars walionyesha kiwango cha hali ya juu na kutawala mchezo huo kuanzia dakika ya kwanza hadi kumpiga mpinzani wake mweleka mzito nyumbani kwake.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa mshambuliaji, Mathew Tegisi, aliyeweka rekodi ya kufunga 'hat-trick' ya mapema ndani ya kipindi cha kwanza.

Tegisi alifungua akaunti ya mabao katika dakika ya 20, kabla ya kuongeza mabao mengine mtawalia katika dakika za 23 na 32.

Kiungo mshambuliaji, Sheikhan Ibrahim, alihitimisha karamu ya mabao ya kipindi cha kwanza kwa kufunga bao la nne katika dakika ya 41, na kupeleka timu hizo mapumziko huku Singida wakiwa mbele kwa mabao 4-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji Al Ghazala wakijaribu kufanya mabadiliko yaliyowasaidia kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Mohammed Zakariya katika dakika ya 70.

Hata hivyo, bao hilo halikuwakatisha tamaa miamba hiyo ya Singida kwani walirudi mchezoni na kupachika mabao mengine kupitia kwa Jonathan Sowah aliyefunga katika dakika za 63 na 90, huku Henry David akipachika bao lingine katika dakika ya 86 na kukamilisha idadi ya mabao saba.

Ushindi huo wa mabao 7-1 unaiweka Singida Black Stars katika nafasi nzuri ya kutinga hatua inayofuata, huku mchezo wa marudiano ukitazamiwa kupigwa nchini Tanzania kati ya Septemba 11 na 13, 2026.

Kama Singida BS itafanikiwa kusonga mbele, itakutana na mshindi kati ya Al Ahli Madani ya Sudan na Tusker FC ya Kenya katika raundi ya pili ya hatua ya kufuzu makundi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Kenya yatangaza uzinduzi wa uwanja wa Raila Odinga kwa mechi ya Bayern Munich na Ajax
Kenya yatangaza uzinduzi wa uwanja wa Raila Odinga kwa mechi ya Bayern Munich na Ajax
2h ago
READ MORE →
Yanga yaangukia kundi B, Simba kundi C CAFCL
Yanga yaangukia kundi B, Simba kundi C CAFCL
6h ago
READ MORE →
Singida Black stars yapangwa kundi C, kukutana na wapinzani wenye uzoefu Afrika
Singida Black stars yapangwa kundi C, kukutana na wapinzani wenye uzoefu Afrika
7h ago
READ MORE →
Azam kukutana na Mayele na Okello kundi B kombe la shirikisho
Azam kukutana na Mayele na Okello kundi B kombe la shirikisho
8h ago
READ MORE →
Manqoba kuvuna milioni 159 baada ya kuachwa na Yanga
Manqoba kuvuna milioni 159 baada ya kuachwa na Yanga
8h ago
READ MORE →
Manqoba Mngqithi ahisi hujuma zilichangia kuondoka kwake Yanga SC
Manqoba Mngqithi ahisi hujuma zilichangia kuondoka kwake Yanga SC
9h ago
READ MORE →
Droo ya CAF Champions League na Confederation cup 2026/27 kufanyika leo
Droo ya CAF Champions League na Confederation cup 2026/27 kufanyika leo
10h ago
READ MORE →
Simba SC yatamani kukutana na RS Berkane au Espérance de Tunis CAF Champions League
Simba SC yatamani kukutana na RS Berkane au Espérance de Tunis CAF Champions League
13h ago
READ MORE →
Fleetwood Town yawaondoa Arsenal EFL Cup, huku tukio la ajabu laonekana angani
Fleetwood Town yawaondoa Arsenal EFL Cup, huku tukio la ajabu laonekana angani
21h ago
READ MORE →
Dodoma Jiji na JKT Tanzania zagawana pointi, nafasi za juu zakaza NBC Premier League
Dodoma Jiji na JKT Tanzania zagawana pointi, nafasi za juu zakaza NBC Premier League
23h ago
READ MORE →