Wachezaji wa Singida Black Stars wamewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Juba, nchini Sudan Kusini, tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam baada ya kumaliza majukumu yao katika nchi hiyo.
Singida Black Stars ilikuwa nchini Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wa mashindano ya CAF dhidi ya Al Ghazala Wau, ambapo kikosi hicho kiliwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Baada ya kukamilisha mchezo huo, kikosi cha Singida sasa kimeanza safari ya kurejea nchini, huku wachezaji na benchi la ufundi wakielekea Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michezo ijayo.