Azam FC imeanza vyema kwenye NBC Premier League baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC. Hassan Mubiru aliipatia Azam FC bao la kwanza dakika ya 28, kabla ya Gibril Sillah kufunga bao la pili dakika ya 90+3 na kukamilisha ushindi huo.
Sillah ameendelea na mwendelezo mzuri baada ya kurejea uwanjani kufuatia kufutiwa adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kimakosa katika mchezo uliopita.
Sasa Azam FC itahamia kwenye mchezo mwingine mgumu wa NBC Premier League, ambapo itakutana na Simba SC Jumatano hii katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Azam FC 2-0 Namungo FC, pointi tatu muhimu kwa Wana-Lamba Lamba, huku macho sasa yakielekezwa kwenye kibarua dhidi ya Simba.