TRA United imefanya uamuzi wa kumuondoa kazini kocha wao Etienne Ndayiragije, kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu katika kipindi cha hivi karibuni.
Leo, uongozi wa TRA United ulikutana katika kikao kizito cha kutathmini hali ya timu, ambapo kikao hicho kimehitimishwa kwa uamuzi wa kuachana na Ndayiragije.
Kocha huyo sasa anaondoka kwenye benchi la TRA United, huku uongozi ukitarajiwa kuchukua hatua zaidi kuhakikisha timu inarejea kwenye mwenendo mzuri wa matokeo.