International, Normal News, UEFA, LASK, Aston Villa, Club Brugge, Manchester City, Borrussia Dortmund, Real Madrid, Inter Milan

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: matokeo ya usiku huu.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
โ€ข
2h ago
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: matokeo ya usiku huu.

Michezo ya saa 1:30 usiku imekamilika kwa AEK Athens kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya LASK, bao pekee likifungwa na Razvan Marin dakika ya 21. Katika mchezo mwingine, Aston Villa imepata ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Club Brugge. McGinn aliifungia Villa dakika ya 11, Buendia akaongeza la pili dakika ya 22, huku Jackson akifunga bao la ushindi dakika ya 43. Club Brugge walipata mabao yao kupitia Vetlesen dakika ya 19 na Tresold kwa mkwaju wa penalti dakika ya 61.Michezo ya saa 4:00 usiku nayo imeleta burudani kubwa, huku Borussia Dortmund ikiifunga Villarreal 3-2. Dortmund ilipata mabao kupitia Veiga dakika ya 53 kwa kujifunga, Guirassy dakika ya 80 na penalti dakika ya 85. Villarreal walijibu kupitia Mourino dakika ya 66, kabla ya Guirassy kujifunga mwenyewe dakika ya 90+3.Manchester City imeondoka Porto na ushindi wa 2-0, ikiwa ni matokeo yaliyotokana na mabao ya Erling Haaland dakika ya 47 na 90+1. Porto imekuwa na usiku mgumu mbele ya lango, kwani haikuweza kupiga hata shuti moja lililolenga lango katika mchezo huo.Nchini Ufaransa, Real Betis imeifunga Lille 3-2 katika mchezo wa mabao mengi. Lille ilianza kwa mabao ya Ueda dakika ya 12 na Alexsandro dakika ya 36, lakini Betis ikageuza mchezo kupitia Bartra aliyefunga dakika ya 33 na 49, kabla ya Parrott kuongeza bao la tatu dakika ya 53. Lille pia ilimaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya Ethan Mbappé kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 56.

BIG MATCH: Real Madrid 2-1 Inter Milan. Real Madrid imeibuka na ushindi muhimu dhidi ya Inter Milan, huku Kylian Mbappé akifungua ukurasa wa mabao dakika ya 14 na Federico Valverde kuongeza la pili dakika ya 23. Inter ilipata bao la kufutia machozi kupitia Augusto dakika ya 77, lakini Los Blancos wakalinda ushindi wao hadi filimbi ya mwisho.Usiku mwingine wenye matokeo makubwa kwenye Champions League, huku Real Madrid na Manchester City zikitoka na pointi tatu muhimu katika michezo yao.

More Stories

Gamondi aenda Simba kujenga ushirikiano na TFF
Gamondi aenda Simba kujenga ushirikiano na TFF
12h ago
READ MORE โ†’
Pacome Zouzoua sehemu ya jeshi la yanga ikiingamiza Gaborone
Pacome Zouzoua sehemu ya jeshi la yanga ikiingamiza Gaborone
14h ago
READ MORE โ†’
Yanga yatangaza โ€œSele Dayโ€ kumkaribisha Selemani Mwalimu Jangwani
Yanga yatangaza โ€œSele Dayโ€ kumkaribisha Selemani Mwalimu Jangwani
15h ago
READ MORE โ†’
Yanga yafungua milango azam complex, viingilio dhidi ya Gaborone vyatajwa
Yanga yafungua milango azam complex, viingilio dhidi ya Gaborone vyatajwa
15h ago
READ MORE โ†’
Hersi ajibu tuhuma za kumlazimisha Chama Yanga
Hersi ajibu tuhuma za kumlazimisha Chama Yanga
16h ago
READ MORE โ†’
Rasmi: UEFA yaagiza dakika moja ya ukimya kwa Nepal.
Rasmi: UEFA yaagiza dakika moja ya ukimya kwa Nepal.
16h ago
READ MORE โ†’
Rasmi: TRA yamfuta kazi kocha Etienne Ndayiragije.
Rasmi: TRA yamfuta kazi kocha Etienne Ndayiragije.
1d ago
READ MORE โ†’
Azam Fc yabeba points tatu NBC Premier League mbele ya Namungo.
Azam Fc yabeba points tatu NBC Premier League mbele ya Namungo.
1d ago
READ MORE โ†’
Tevez kuvunja mwiko, Messi na Ronaldo kucheza timu moja
Tevez kuvunja mwiko, Messi na Ronaldo kucheza timu moja
1d ago
READ MORE โ†’