Local, Normal News, Yanga Sc

Manqoba anautaka ubingwa Afrika

Joel JJ By Joel JJ
โ€ข
3h ago
Manqoba anautaka ubingwa Afrika

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, pamoja na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, wameweka wazi mipango na mikakati ya kikosi hicho kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Gaborone United.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Yanga Media Day iliyofanyika mapema leo, Mngqithi amesema Yanga haijaingia katika mashindano hayo kwa lengo la kushiriki pekee, bali ina dhamira ya kupambana hadi kufikia hatua ya juu zaidi na hatimaye kutwaa ubingwa wa Afrika.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema kikosi chake kinaendelea kuimarika siku hadi siku na anaamini kina ubora wa kutosha kushindana na timu kubwa barani Afrika.

“Malengo yetu ni makubwa; tunataka ubingwa wa Afrika na tuna kikosi chenye uwezo wa kupambana kufikia hatua hiyo. Niwaombe mashabiki wetu wasiwe na hofu, waje kwa wingi uwanjani kutusapoti kwani timu ipo imara,” alisema Mngqithi.

Kwa upande wake, Ali Kamwe amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa Yanga kuelekea mchezo huo dhidi ya Gaborone United, akisisitiza kuwa licha ya kuwa mchezo mgumu, wapinzani wao si wa kiwango cha kuwatisha kiasi cha kuzuia Yanga kusonga mbele.

Kamwe amebainisha kuwa moja ya maeneo ambayo benchi la ufundi limeyapa kipaumbele ni mipira ya kutenga (set pieces), ambayo amesema Gaborone United imekuwa na nguvu nayo.

“Ni mchezo mgumu lakini sio wa kutisha. Tunajua mpinzani wetu ana silaha kubwa kwenye mipira ya kutenga (set pieces), na benchi letu la ufundi chini ya Kocha Mngqithi, ambaye ana uzoefu mkubwa sana na mashindano haya ya Afrika, limeyafanyia kazi hayo yote,” alisema Kamwe.

Aidha, Kamwe amesisitiza umuhimu wa mashabiki katika mchezo huo, akieleza kuwa nguvu kubwa ya Yanga inatarajiwa kutoka jukwaani.

Amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, siku ya Jumamosi, ili kuipa timu hamasa na kutengeneza mazingira magumu kwa wapinzani wao.

Kamwe azungumzia Aziz Ki

Akizungumzia pia hali ya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, Kamwe amesema mchezaji huyo bado ni sehemu muhimu ya kikosi cha Yanga na anaendelea kuwa tegemeo katika mipango ya timu.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa maamuzi kuhusu matumizi ya mchezaji yeyote uwanjani yanafanywa kwa kuzingatia utimamu wa mchezaji, mahitaji ya timu na mikakati ya kocha, badala ya kuangalia ukubwa wa jina la mchezaji.

More Stories

Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
3h ago
READ MORE โ†’
Rasmi: Hemed Suleiman โ€œMoroccoโ€ ametangazwa kocha mpya wa TRA United
Rasmi: Hemed Suleiman โ€œMoroccoโ€ ametangazwa kocha mpya wa TRA United
3h ago
READ MORE โ†’
Uefa champions League: matokeo ya mechi 6 za kibabe leo.
Uefa champions League: matokeo ya mechi 6 za kibabe leo.
21h ago
READ MORE โ†’
Clara Luvanga aweka historia Marekani, asajiliwa kwa rekodi Tanzania
Clara Luvanga aweka historia Marekani, asajiliwa kwa rekodi Tanzania
1d ago
READ MORE โ†’
Gamondi ateta na viongozi, benchi la ufundi Yanga
Gamondi ateta na viongozi, benchi la ufundi Yanga
1d ago
READ MORE โ†’
Kimoto akalia kuti kavu baada ya kipigo dhidi ya Mashujaa Fc
Kimoto akalia kuti kavu baada ya kipigo dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE โ†’
Chama aweka wazi kinachoendelea nje ya uwanja, si sehemu ya maisha yangu
Chama aweka wazi kinachoendelea nje ya uwanja, si sehemu ya maisha yangu
1d ago
READ MORE โ†’
Doumbia akiri mambo magumu, haijawahi kutokea
Doumbia akiri mambo magumu, haijawahi kutokea
1d ago
READ MORE โ†’
Morocco apindua meza TRA United, kumrithi Ndayirajige
Morocco apindua meza TRA United, kumrithi Ndayirajige
1d ago
READ MORE โ†’