Winga wa Simba SC, raia wa Senegal Libasse Gueye, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Agosti katika NBC Premier League, baada ya kuwashinda wapinzani wake Oscar Mwajanga wa Mbeya City na Maxi Nzengeli wa Yanga SC waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Gueye amefanya vizuri katika mwezi huo, akionyesha kiwango bora na kuwa miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa Simba katika michezo ya ligi.
Katika mwezi wa Agosti, Libasse amehusika moja kwa moja katika mabao sita ya Simba, akifanikiwa kutoa assist tano huku akifunga bao moja.
Tuzo hiyo inaendelea kuonyesha namna winga huyo alivyoanza kuleta ushawishi katika kikosi cha Simba, hasa kwenye kutengeneza nafasi na kuwaunganisha washambuliaji na mabao.
Kwa upande mwingine, Oscar Mwajanga na Maxi Nzengeli walitoa ushindani katika kinyang’anyiro hicho, lakini kura na tathmini za mwezi huo zimempa ushindi Libasse Gueye..jpg)