Michuano ya CAF Champions League inaendelea leo, ambapo Yanga SC itakuwa dimbani kuikabili Gaborone United ya Botswana.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku, huku Yanga ikilenga kupata matokeo mazuri katika hatua hii ya michuano.
Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga katika safari yake ya kuwania nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano makubwa zaidi ya klabu barani Afrika.