Local, Normal News, CAFCL, Yanga, Gaborone United

Yanga yaichapa Gaborone United 2-1 Azam Complex

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2h ago
Yanga yaichapa Gaborone United 2-1 Azam Complex

Yanga SC imefanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Haukuwa mchezo mwepesi kwa Wananchi, ambao walilazimika kupambana hadi filimbi ya mwisho ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi huo mbele ya mashabiki wao.

Yanga ilianza kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya saba kupitia mshambuliaji wake Peter Shalulile, aliyemalizia pasi nzuri kutoka kwa Selemani Mwalimu, ambaye alipokea mpira uliotengenezwa na Stephane Aziz Ki.

Baada ya bao hilo, Yanga iliendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa za kuongeza uongozi. Selemani Mwalimu alikosa nafasi nzuri ambayo ingeweza kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa na zaidi ya bao moja.

Kipindi cha pili, Gaborone United walirejea uwanjani wakiwa na mpango wa kusaka bao la kusawazisha. Wakati huo huo, Yanga iliendelea kutengeneza nafasi, lakini uimara wa kipa wa Gaborone United uliwazuia Wananchi kuongeza mabao.

Mabadiliko ya Yanga yalionekana kuipa Gaborone nafasi ya kusukuma mashambulizi zaidi. Stephane Aziz Ki na Peter Shalulile walitolewa, nafasi zao zikichukuliwa na Hussein Zakouane na Albert Kangwanda, huku Mwalimu akibaki akiongoza safu ya ushambuliaji.

Mabadiliko hayo yaliwapa Gaborone United nafasi ya kutawala zaidi mchezo na kuiwekea Yanga presha katika dakika za mwisho.

Hata hivyo, Yanga ilipata bao la pili dakika ya 83 kupitia Cheick Ibrahim Toure, aliyeingia kuchukua nafasi ya Mwalimu. Toure alimalizia kazi nzuri iliyoanzishwa na Albert Kangwanda na kuifanya Yanga kuongoza 2-0.

Gaborone United hawakukata tamaa na walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 86. Bao hilo liliiongezea Yanga presha kubwa katika dakika za lala salama, huku wageni wakisaka bao la kusawazisha.

Licha ya presha hiyo, Yanga iliweza kulinda uongozi wake hadi filimbi ya mwisho na kushinda 2-1.

Kwa matokeo hayo, Yanga imefuzu raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

More Stories

Yanga yatinga hatua inayofuata CAF baada ya kuiondoa Gaborone United
Yanga yatinga hatua inayofuata CAF baada ya kuiondoa Gaborone United
2h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 2-1 Gaborone United
Highlights : Yanga 2-1 Gaborone United
2h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza ubabe dhidi ya Mighty Wonderers
Barker apania kuendeleza ubabe dhidi ya Mighty Wonderers
10h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 25, Septemba 12 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 25, Septemba 12 2026
11h ago
READ MORE β†’
EPL leo: mechi saba za kibabe
EPL leo: mechi saba za kibabe
12h ago
READ MORE β†’
CAF Champions league kuendelea leo
CAF Champions league kuendelea leo
12h ago
READ MORE β†’
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1d ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
1d ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
1d ago
READ MORE β†’