Local, Normal News, Simba SC, Libasse Gueye

Libasse Gueye aendelea kuwa winga tishio kubwa kwenye soka la Tanzania

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
2h ago
Libasse Gueye aendelea kuwa winga tishio kubwa kwenye soka la Tanzania

Kwa sasa nchini Tanzania, ukiachana na Pacome Zouzoua, ambaye yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha, Libasse Gueye anaonekana kuwa miongoni mwa mawinga hatari na machachari zaidi kwenye soka la Tanzania.

Gueye si mchezaji anayehusika na kutengeneza nafasi pekee, bali ana uwezo mkubwa wa kutoa assist pamoja na kufunga mabao, jambo linalomfanya kuwa tishio la muda wote kwa safu za ulinzi za wapinzani.

Mwinga huyo amekuwa akionyesha uwezo wa kutumia kasi, ujanja na ubunifu wake kuvuruga mipango ya mabeki, huku uwezo wake wa kucheza katika maeneo tofauti ya safu ya ushambuliaji ukimpa thamani zaidi kwenye kikosi.

Kwa upande wa Simba SC, Gueye amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu na tegemezi katika kikosi.

Uwepo wake umeendelea kuwa na mchango mkubwa katika namna Simba inavyoshambulia na kutengeneza nafasi za kufunga.

Mara kadhaa imeonekana kwamba pale Gueye anapokosekana kwenye mchezo, Simba hupata changamoto zaidi katika kutengeneza nafasi, kuongeza kasi kwenye mashambulizi na kupata matokeo mazuri.

Hali hiyo inaonyesha umuhimu wake ndani ya kikosi na kwa nini wapinzani wamekuwa wakihitaji kuwa makini zaidi wanapokutana na Simba akiwa kwenye kiwango chake.

Kwa uwezo wake wa kufunga, kutoa assist na kuvuruga safu za ulinzi, Libasse Gueye anaendelea kujitengenezea nafasi miongoni mwa mawinga wanaohitaji uangalizi mkubwa kwenye soka la Tanzania kwa sasa.

More Stories

Caf yaendelea kukuza soka la afrika, klabu zilizotoka mapema zalipwa dola lakimoja
Caf yaendelea kukuza soka la afrika, klabu zilizotoka mapema zalipwa dola lakimoja
16m ago
READ MORE β†’
Pro ref yakiri kosa bao la haaland lililoipa Man City ushindi dhidi ya united
Pro ref yakiri kosa bao la haaland lililoipa Man City ushindi dhidi ya united
1h ago
READ MORE β†’
Hatua za mwisho kabla ya kuingia makundi ya CAF, Simba, Yanga, Azam Singida Bs kukutana na hawa
Hatua za mwisho kabla ya kuingia makundi ya CAF, Simba, Yanga, Azam Singida Bs kukutana na hawa
13h ago
READ MORE β†’
TRA United Yaibuka na Ushindi Chini ya Hemed Suleiman.
TRA United Yaibuka na Ushindi Chini ya Hemed Suleiman.
13h ago
READ MORE β†’
Manchester city yaishangaza united, yashinda derby old trafford
Manchester city yaishangaza united, yashinda derby old trafford
14h ago
READ MORE β†’
Simba yaiadhibu Mighty Wanderers 6-1, yafuzu raundi ya kwanza kibabe
Simba yaiadhibu Mighty Wanderers 6-1, yafuzu raundi ya kwanza kibabe
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Simba 6-1 Mighty Wonderers
Highlights : Simba 6-1 Mighty Wonderers
18h ago
READ MORE β†’
EPL leo: mechi mbili za moto, Manchester derby kutafutwa mbabe
EPL leo: mechi mbili za moto, Manchester derby kutafutwa mbabe
23h ago
READ MORE β†’
Simba kuumana na Mighty wanderers leo uwanja wa uhuru
Simba kuumana na Mighty wanderers leo uwanja wa uhuru
1d ago
READ MORE β†’