Local, Normal News, Chipolopolo, Zambia, Kangwanda, Yanga, Tanzania, Afcon 2027

Kangwanda aitwa chipolopolo kufuzu afcon 2027

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
39m ago
Kangwanda aitwa chipolopolo kufuzu afcon 2027

Kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Zambia, George Lwandamina, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu AFCON 2027, huku mshambuliaji wa Yanga SC, Albert Kangwanda, akiwa miongoni mwa walioitwa katika kikosi hicho.

Zambia itaanza kampeni hizo kwa kucheza dhidi ya Algeria ugenini Septemba 25, 2026, kabla ya kurejea nyumbani Septemba 29 kukabiliana na Togo katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola. Zambia ipo Kundi I pamoja na Algeria, Togo na Burundi.

Kangwanda amejumuishwa katika safu ya washambuliaji pamoja na nyota wengine kama Patson Daka wa Hamburg, Fashion Sakala wa Al Fayha na Kingston Mutandwa wa Servette.

Kwa Kangwanda, wito huo unampa nafasi ya kuendelea kuiwakilisha Zambia katika hatua ya kimataifa, huku akiwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kusaidia Chipolopolo katika harakati za kuwania nafasi ya kushiriki AFCON 2027, ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

More Stories

Mngqithi Atoa Kauli Kabla ya Yanga Kuikabili Geita Gold
Mngqithi Atoa Kauli Kabla ya Yanga Kuikabili Geita Gold
1h ago
READ MORE β†’
Lamine yamal: sitalala, nataka kuandika historia ya soka
Lamine yamal: sitalala, nataka kuandika historia ya soka
1h ago
READ MORE β†’
Caf yaendelea kukuza soka la afrika, klabu zilizotoka mapema zalipwa dola lakimoja
Caf yaendelea kukuza soka la afrika, klabu zilizotoka mapema zalipwa dola lakimoja
3h ago
READ MORE β†’
Pro ref yakiri kosa bao la haaland lililoipa Man City ushindi dhidi ya united
Pro ref yakiri kosa bao la haaland lililoipa Man City ushindi dhidi ya united
4h ago
READ MORE β†’
Libasse Gueye aendelea kuwa winga tishio kubwa kwenye soka la Tanzania
Libasse Gueye aendelea kuwa winga tishio kubwa kwenye soka la Tanzania
4h ago
READ MORE β†’
Hatua za mwisho kabla ya kuingia makundi ya CAF, Simba, Yanga, Azam Singida Bs kukutana na hawa
Hatua za mwisho kabla ya kuingia makundi ya CAF, Simba, Yanga, Azam Singida Bs kukutana na hawa
16h ago
READ MORE β†’
TRA United Yaibuka na Ushindi Chini ya Hemed Suleiman.
TRA United Yaibuka na Ushindi Chini ya Hemed Suleiman.
16h ago
READ MORE β†’
Manchester city yaishangaza united, yashinda derby old trafford
Manchester city yaishangaza united, yashinda derby old trafford
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaiadhibu Mighty Wanderers 6-1, yafuzu raundi ya kwanza kibabe
Simba yaiadhibu Mighty Wanderers 6-1, yafuzu raundi ya kwanza kibabe
20h ago
READ MORE β†’