Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtangaza Herry Sasii kutoka Dar es Salaam kuwa mwamuzi wa mchezo wa leo wa NBC Premier League kati ya Azam FC na Simba SC, unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa katika pambano la Mzizima Derby.
Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, Sasii atasaidiwa na Jesse Erasmos kutoka Morogoro pamoja na Khamis Changβwalu kutoka Dar es Salaam.
Hance Mabena kutoka Tanga ameteuliwa kuwa mwamuzi wa akiba, wakati nafasi ya kamishna wa mchezo imekwenda kwa Abubakary Kazinja kutoka Kagera.
Uteuzi wa waamuzi hao unakuja wakati Azam FC na Simba SC zikitarajiwa kukutana katika mchezo ambao unavuta hisia kubwa za mashabiki wa soka nchini.
Macho yataelekezwa pia kwa Herry Sasii na wasaidizi wake kuhakikisha mchezo unasimamiwa kwa kuzingatia sheria za mchezo, huku kila upande ukitafuta matokeo muhimu katika Mzizima Derby.