International, Normal News, Laliga, Barcelona, Sevilla

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
2h ago
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.

Barcelona imeendeleza mwanzo wake mzuri wa msimu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sevilla, huku mshambuliaji wa Brazil, Raphinha, akiwa nyota wa mchezo baada ya kufunga hat-trick na kuendeleza rekodi yake ya kuvutia katika kila mchezo aliocheza msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amehusika moja kwa moja katika bao angalau moja katika kila mechi ya Barcelona msimu huu. Katika michezo nane, Raphinha amefikisha mabao 14, ikiwa ni pamoja na hat-trick mbili mfululizo ndani ya muda wa saa 72, kiwango kinachoendelea kumfanya kuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Hansi Flick.

Hat-trick dhidi ya Sevilla imekuja baada ya Raphinha pia kufunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya Racing Santander. Kabla ya hapo alifunga mara mbili dhidi ya Elche, mara moja dhidi ya Athletic Club, mara mbili dhidi ya Rayo Vallecano, mara moja dhidi ya Valencia na mara mbili dhidi ya Feyenoord, huku akitoa pia pasi mbili za mabao dhidi ya Levante.Mwanzo huu wa Raphinha umekuwa wa kipekee kutokana na mazingira ya kikosi cha Barcelona, baada ya klabu hiyo kumpoteza Robert Lewandowski na Ferran Torres katika majira ya kiangazi na kushindwa kumnasa Julián Álvarez. Hali hiyo ilimfanya Flick kumtumia Raphinha katika nafasi ya mshambuliaji wa kati, uamuzi ambao umeonekana kumpa nafasi ya kuendelea kuonyesha uwezo wake wa kufunga mabao.

Ushindi dhidi ya Sevilla umeendeleza pia rekodi ya Barcelona ya kushinda kila mchezo wa mashindano yote msimu huu chini ya Hansi Flick. Raphinha akiwa moto, Lamine Yamal akitoa pasi mbili za mabao, Barcelona inaendelea kutoa onyesho jingine la kuvutia.

More Stories

Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
6h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
6h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
9h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
15h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
15h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’