Local, Normal News, Namungo, Mgunda, Ligi kuu bara, TFF

Juma Mgunda: Kujenga timu mpya kunahitaji muda na subira

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
โ€ข
1h ago
Juma Mgunda: Kujenga timu mpya kunahitaji muda na subira

Kocha wa Namungo FC, Juma Mgunda, amesema ujenzi wa kikosi kipya unahitaji muda na subira, akieleza kuwa timu yake haikupata muda wa kutosha wa maandalizi ya msimu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara 2026/27.

Mgunda amesema mabadiliko ya kikosi na kuwasajili wachezaji wapya yanahitaji muda ili wachezaji wafahamiane, waelewe mfumo wa uchezaji na kujenga maelewano uwanjani. “Unapotengeneza timu mpya unahitaji muda na subira, kwa sababu mpira ni process, siyo kama unaweka chumvi kwenye mboga halafu ikakolea mara moja. Ni mchakato wa hatua kwa hatua,” amesema.

Kocha huyo amesema changamoto hiyo imeongezwa na ratiba ya msimu, baada ya ligi iliyopita kumalizika kwa kuchelewa huku msimu mpya ukianza mapema, hali iliyopunguza muda wa maandalizi ya pre-season. Kwa sasa, amesema Namungo inatumia kipindi cha mapumziko cha wiki tatu kama semi pre-season kurekebisha mapungufu na makosa yaliyoonekana katika michezo ya mwanzo.

Namungo imecheza mechi saba za ligi, ikishinda mbili na kupoteza tano, ikiwa na pointi sita na kukaa nafasi ya 13 kwenye msimamo. Mgunda anatumia muda uliopo kuimarisha kikosi hicho kabla ya kurejea kwenye ushindani wa ligi.

More Stories

Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
1m ago
READ MORE โ†’
Fiston Mayele awasili kambini DR Congo kwa ajili ya kufuzu AFCON 2027
Fiston Mayele awasili kambini DR Congo kwa ajili ya kufuzu AFCON 2027
13m ago
READ MORE โ†’
Kudus ajiondoa kikosi cha Ghana kuelekea mechi za kufuzu Afcon 2027
Kudus ajiondoa kikosi cha Ghana kuelekea mechi za kufuzu Afcon 2027
47m ago
READ MORE โ†’
Manchester City yaichapa Sunderland 5โ€“3 katika mechi ya mabao nane
Manchester City yaichapa Sunderland 5โ€“3 katika mechi ya mabao nane
16h ago
READ MORE โ†’
Atletico yangโ€™ara kwenye dabi, Real Madrid aangukia pua ugenini
Atletico yangโ€™ara kwenye dabi, Real Madrid aangukia pua ugenini
16h ago
READ MORE โ†’
Nyota Geita Gold afunguka rafu ya Aziz KI, Ilikuwa bahati mbaya
Nyota Geita Gold afunguka rafu ya Aziz KI, Ilikuwa bahati mbaya
22h ago
READ MORE โ†’
LAPORTA: Atletico kumuuza Alvarez kwa timu yeyote isipokuwa Barcelona
LAPORTA: Atletico kumuuza Alvarez kwa timu yeyote isipokuwa Barcelona
1d ago
READ MORE โ†’
Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
1d ago
READ MORE โ†’
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
1d ago
READ MORE โ†’