Local, Normal News, Sandaland, Makonda, TFF, Taifa stars, Jezi

Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
54m ago
Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia

Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kauli yake kuhusu jezi mpya za Taifa Stars.

Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda, Septemba 16, 2026, kuchapisha ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram akieleza kutoridhishwa na jezi hizo na kuhoji matumizi ya picha ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, katika kuziwasilisha kwa umma.

Katika taarifa yake, Sandaland imesema kauli hiyo imeathiri jina, chapa na hadhi ya kampuni, huku ikisisitiza kuwa ina mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi za Taifa Stars. Kampuni hiyo pia imedai kuwa tayari imeanza kuona madhara ya kiuchumi na kihadhi kutokana na kauli hiyo.

Sandaland imesema haitakaa kimya na inakusudia kuchukua hatua za kisheria kuhusu kauli hiyo, huku ikitaka suala hilo lishughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Mzozo huo sasa unaendelea huku kukiwa na misimamo tofauti kuhusu jezi hizo, mkataba wa TFF na namna zilivyowasilishwa kwa umma.

More Stories

Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
2h ago
READ MORE β†’
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
3h ago
READ MORE β†’
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
18h ago
READ MORE β†’
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
19h ago
READ MORE β†’
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
22h ago
READ MORE β†’
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
22h ago
READ MORE β†’
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
23h ago
READ MORE β†’
Tumejipanga vizuri kukabiliana dhidi ya Kenya AFCON 2027 - Ahmad Ally
Tumejipanga vizuri kukabiliana dhidi ya Kenya AFCON 2027 - Ahmad Ally
1d ago
READ MORE β†’
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza
1d ago
READ MORE β†’