Local, Normal News, Rushine, Simba, South afrca, Cape town , Ligi kuu bara, Nguvu moja

Rushine De Reuck afunguka mazito ya utotoni, Wengine wapo jela wengine wameshakufa

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
1h ago
Rushine De Reuck afunguka mazito ya utotoni, Wengine wapo jela wengine wameshakufa

Mlinzi na nahodha msaidizi wa Simba SC, Rushine De Reuck, amefunguka kuhusu mazingira magumu aliyokulia katika eneo la Cape Flats, Cape Town nchini Afrika Kusini, akieleza kuwa uhalifu, dawa za kulevya na magenge yalikuwa sehemu ya changamoto za maisha ya eneo hilo.

De Reuck, ambaye alizaliwa na kukulia Kalksteenfontein, amesema baadhi ya watu aliokua nao tangu utotoni walijikuta wakiingia katika maisha ya uhalifu, huku wengine wakifungwa na wengine kupoteza maisha kutokana na matukio yanayohusishwa na uhalifu.

“Wenzangu ambao tulikuwa pamoja tangu tukiwa wadogo, leo hii wapo jela na wengine wameshakufa kwa matukio ya kihalifu,” alisema De Reuck.

Akizungumza kuhusu namna alivyoweza kuiepuka hali hiyo, De Reuck ameeleza kuwa soka lilikuwa sehemu muhimu iliyomsaidia kubadilisha mwelekeo wa maisha yake na kumpa fursa ya kufikia hatua ya kuwa mchezaji wa kulipwa. “Nashukuru Mungu kwa kunipa kipaji cha mpira. Kimenitoa na kuniweka katika ulimwengu tofauti,” aliongeza.

De Reuck, ambaye kabla ya kujiunga na Simba aliwahi kuitumikia Mamelodi Sundowns, amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Simba tangu kuwasili kwake Tanzania.

More Stories

Hersi: Yanga imempoteza kiongozi mkubwa
Hersi: Yanga imempoteza kiongozi mkubwa
1h ago
READ MORE β†’
Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia
Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia
2h ago
READ MORE β†’
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
4h ago
READ MORE β†’
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
5h ago
READ MORE β†’
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
20h ago
READ MORE β†’
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
21h ago
READ MORE β†’
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
1d ago
READ MORE β†’
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
Zakaria Thabit afunguka kuhusu mwanzo wa msimu wa Azam FC
1d ago
READ MORE β†’
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
Kagera Sugar yafukuza benchi zima la ufundi!
1d ago
READ MORE β†’