Local, Normal News, Sandaland, TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

TFF yakerwa na matumizi ya nembo yake kwenye mkataba wa Sandaland

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
1h ago
TFF yakerwa na matumizi ya nembo yake kwenye mkataba wa Sandaland

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeeleza kusikitishwa na matumizi ya nembo yake katika mkataba na waandishi ulioandaliwa na kampuni ya Sandaland Fashion Wear.

TFF imesema haikuhusika wala haikushirikishwa katika maandalizi ya mkataba huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa TFF, matumizi ya nembo yake katika maudhui ambayo hayana uhusiano wa kimkataba kati ya shirikisho hilo na Sandaland Fashion Wear hayaruhusiwi.

TFF imeonya kampuni hiyo kuacha kutumia nembo ya shirikisho katika nyaraka au maudhui ambayo hayahusiani na makubaliano rasmi kati ya pande hizo mbili.

Aidha, TFF imeeleza kuwa itaandika barua kwa Sandaland Fashion Wear ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu sababu na namna nembo ya shirikisho ilivyotumika katika mkataba huo.

Hatua hiyo inafuatia mkataba huo kuonekana ukiwa na nembo ya TFF, jambo ambalo limeibua maelezo rasmi kutoka kwa shirikisho hilo.

More Stories

Ngorongoro Heroes yakata tiketi Afcon U20 baada ya ushindi dhidi ya Burundi
Ngorongoro Heroes yakata tiketi Afcon U20 baada ya ushindi dhidi ya Burundi
2h ago
READ MORE β†’
Rushine De Reuck afunguka mazito ya utotoni, Wengine wapo jela wengine wameshakufa
Rushine De Reuck afunguka mazito ya utotoni, Wengine wapo jela wengine wameshakufa
6h ago
READ MORE β†’
Hersi: Yanga imempoteza kiongozi mkubwa
Hersi: Yanga imempoteza kiongozi mkubwa
6h ago
READ MORE β†’
Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia
Sandaland yatoa msimamo wao kwa Waziri Makonda, Yadai radhi na fidia
8h ago
READ MORE β†’
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
Nyota Taifa Stars watamani uwepo wa Mbwana Samatta
9h ago
READ MORE β†’
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
Barcelona ndiyo timu bora kwa sasa: Simeone
10h ago
READ MORE β†’
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
Simon Msuva awasili rasmi kambini kujiunga na taifa stars
1d ago
READ MORE β†’
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
Kaze amrithi Kaseja Kagera Sugar
1d ago
READ MORE β†’
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
Morgan Gibbs kuchukua nafasi ya Palmer Uingereza
1d ago
READ MORE β†’