Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeeleza kusikitishwa na matumizi ya nembo yake katika mkataba na waandishi ulioandaliwa na kampuni ya Sandaland Fashion Wear.
TFF imesema haikuhusika wala haikushirikishwa katika maandalizi ya mkataba huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa TFF, matumizi ya nembo yake katika maudhui ambayo hayana uhusiano wa kimkataba kati ya shirikisho hilo na Sandaland Fashion Wear hayaruhusiwi.
TFF imeonya kampuni hiyo kuacha kutumia nembo ya shirikisho katika nyaraka au maudhui ambayo hayahusiani na makubaliano rasmi kati ya pande hizo mbili.
Aidha, TFF imeeleza kuwa itaandika barua kwa Sandaland Fashion Wear ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu sababu na namna nembo ya shirikisho ilivyotumika katika mkataba huo.
Hatua hiyo inafuatia mkataba huo kuonekana ukiwa na nembo ya TFF, jambo ambalo limeibua maelezo rasmi kutoka kwa shirikisho hilo.