Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kesho, Alhamisi, Septemba 24, 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Wizara yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo leo, Septemba 23, mkutano huo utajadili pia matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa yanayotarajiwa kufanyika nchini katika mwaka 2026/2027.
Mkutano huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt, Posta, Dar es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi, huku usajili wa waandishi wa habari ukianza saa 2:00 asubuhi.
Wizara imesema waandishi watakaohudhuria watapata fursa ya kumuuliza Waziri Makonda maswali mbalimbali na kupata majibu papo hapo. Miongoni mwa masuala yanayoweza kuibuka ni pamoja na mzozo wa hivi karibuni kuhusu jezi za Taifa Stars, ambao umehusisha kampuni ya Sandaland na Wizara.