Aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, amesema mvutano unaohusisha jezi za Taifa Stars na kampuni ya Sandaland Fashion Wear si jambo lenye afya kwa maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Ndumbaro amesema hayo leo jioni kupitia kipindi cha Jana na Leo kinachorushwa na Wasafi FM, akizungumzia hali ya michezo nchini na umuhimu wa kuwepo kwa mazingira yenye utulivu kuelekea mashindano hayo.
Sakata hilo limeibuka kufuatia mjadala kuhusu jezi mpya za Taifa Stars, huku Wizara ikiwa na msimamo kuhusu mchakato huo.
Kwa upande wake, Sandaland Fashion Wear imeeleza kuwa ina mkataba na TFF wa kuzalisha na kusambaza jezi za timu za taifa.
Ndumbaro amesema mvutano huo hauendani na mazingira yanayohitajika katika maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.