Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Tanzania imejipanga kutumia mashindano ya Miss World 2027 kama fursa ya kutangaza utamaduni wa nchi kimataifa.
Makonda amesema mashindano hayo, ambayo yanatarajiwa kufanyika Tanzania mwaka 2027, yatatoa nafasi ya kuonesha utajiri wa tamaduni za Tanzania, ikiwemo mila na desturi za makabila mbalimbali.
Amesema Tanzania ina zaidi ya makabila 120, hivyo maandalizi ya mashindano hayo yatakuwa fursa ya kuutambulisha utamaduni wa kila kabila kwa dunia, pamoja na kuendeleza na kukuza tamaduni za Tanzania.
Makonda ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam leo, Septemba 25, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, Tanzania inalenga kutumia jukwaa la Miss World 2027 kuonesha utambulisho wake wa kitamaduni na kuwafikisha watu kutoka sehemu mbalimbali duniani karibu na urithi wa Tanzania.