Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club imefanya uteuzi wa wajumbe wa Kamati mbalimbali za klabu hiyo, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuimarisha muundo wa uongozi na uendeshaji wa shughuli za klabu.
Katika kikao kilichofanyika Septemba 23, 2026, Bodi imemteua Anderson David Msumba kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, akisaidiwa na Alpha Honest Gervas kama Makamu Mwenyekiti. Rose Manka Sissya, Richard Daudi Mwalwiba na Jotham Mubelwa Mazima wamechaguliwa kuwa wajumbe.
Kamati ya Nidhamu itaongozwa na Suleiman Hussein Kova akiwa Mwenyekiti, huku Peter Lucas Mwitwa akiwa Makamu Mwenyekiti. Robert Francis Selasela, George Magere Masatu na Racheal Juma Chagonja wamepata nafasi za wajumbe.
Kwa upande wa Kamati ya Maadili, Charles Ndalahwa Kenyela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti, akisaidiwa na Anna Anjibithe Marealle kama Makamu Mwenyekiti, huku George Rwezaura Shumbusho, Aziz Hassan Kifile na Gerald Robert Yambi wakiwa wajumbe. Uteuzi huo unalenga kuimarisha usimamizi wa masuala ya uchaguzi, nidhamu na maadili ndani ya klabu.