Local, Normal News, AFCON 2027, Africa, Tanzania, Zanzibar,

Timu ya taifa ni mali ya nchi, sio kampuni ya mtu - Makonda

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
โ€ข
28m ago
Timu ya taifa ni mali ya nchi, sio kampuni ya mtu - Makonda

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Timu ya Taifa ya Tanzania ni mali ya nchi na si kampuni ya mtu binafsi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Makonda amesema mamlaka ya Waziri katika kusimamia sekta ya michezo yapo kwa mujibu wa Sheria, Sera na Kanuni, akisisitiza kuwa Timu ya Taifa inawakilisha nchi kila inapokwenda.

โ€œTimu ya Taifa ni mali ya Nchi, sio kampuni ya Mtu, ndiyo maana tumeikasimu na kuihudumia, timu ikienda popote pale, ni Nchi inaenda,โ€ amesema Makonda.

Makonda pia amesema Waziri anayesimamia sekta hiyo ni mteule wa Rais, hivyo mamlaka yake yanapaswa kuheshimiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuisimamia sekta ya michezo.

โ€œWanamfanya kama Waziri wanamdharau, lakini huyo ni mteule wa Rais anayesimamia wizara ambayo inakupa mkate,โ€ amesema Makonda.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya michezo na uendeshaji wa Timu ya Taifa nchini.

More Stories

Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027
Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027
9m ago
READ MORE โ†’
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
19m ago
READ MORE โ†’
Simba yapanga safu mpya za uendeshaji, Kamati tatu zateuliwa
Simba yapanga safu mpya za uendeshaji, Kamati tatu zateuliwa
31m ago
READ MORE โ†’
Fedha hazijakwamisha maandalizi ya AFCON 2027 - Makonda
Fedha hazijakwamisha maandalizi ya AFCON 2027 - Makonda
39m ago
READ MORE โ†’
Fainali CECAFA U20 Kupigwa leo, Tanzania kukutana na Sudan
Fainali CECAFA U20 Kupigwa leo, Tanzania kukutana na Sudan
43m ago
READ MORE โ†’
Miss World 2027 kutangaza utamaduni wa Tanzania - Makonda:
Miss World 2027 kutangaza utamaduni wa Tanzania - Makonda:
45m ago
READ MORE โ†’
Van Dijk afichua kilichomfanya aendelee na Uholanzi
Van Dijk afichua kilichomfanya aendelee na Uholanzi
2h ago
READ MORE โ†’
Taifa Stars yaelekea Zanzibar kukutana na Guinea-Bissau
Taifa Stars yaelekea Zanzibar kukutana na Guinea-Bissau
2h ago
READ MORE โ†’
Ahmed Ally aeleza sababu za Simba SC kuweka kambi Afrika Kusini
Ahmed Ally aeleza sababu za Simba SC kuweka kambi Afrika Kusini
2h ago
READ MORE โ†’