Local, Normal News, Tanzania, TFF, Makonda, Afcon 2027, Taifa stars, Uganda, Kenya

Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
21m ago
Serikali yalipa Bilioni 104 kwa ajili ya Afcon 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali ya Tanzania imelipa Shilingi bilioni 104 katika maandalizi na upatikanaji wa haki ya matangazo kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, zitakazofanyika kwa pamoja Tanzania, Kenya na Uganda.

Makonda ameyasema hayo Septemba 24, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya AFCON 2027, Miss World na masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya sanaa. Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuelekea mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027.

Kwa mujibu wa Makonda, Serikali inalenga kutumia AFCON 2027 kama jukwaa la kuitangaza Tanzania kimataifa, sambamba na kukuza sekta ya michezo, utalii na shughuli za kiuchumi zinazohusiana na mashindano hayo.

Maandalizi ya Tanzania yanaendelea katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya michezo. Hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya mwaka wa fedha 2026/27 inaeleza kuwa ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ulikuwa umefikia asilimia 95, huku ujenzi wa uwanja mpya wa Arusha ukiwa umefikia asilimia 77.5 wakati wa taarifa hiyo.

More Stories

Makonda azitaka klabu kutumia vikao vya ndani kutatua migogoro
Makonda azitaka klabu kutumia vikao vya ndani kutatua migogoro
1m ago
READ MORE β†’
Makonda avitaka vilabu kumaliza migogoro yao kwa vikao vya ndani
Makonda avitaka vilabu kumaliza migogoro yao kwa vikao vya ndani
8m ago
READ MORE β†’
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
Gamondi aanza mchakato wa kumpata Nahodha mpya wa Taifa Stars
30m ago
READ MORE β†’
Timu ya taifa ni mali ya nchi, sio kampuni ya mtu - Makonda
Timu ya taifa ni mali ya nchi, sio kampuni ya mtu - Makonda
39m ago
READ MORE β†’
Simba yapanga safu mpya za uendeshaji, Kamati tatu zateuliwa
Simba yapanga safu mpya za uendeshaji, Kamati tatu zateuliwa
42m ago
READ MORE β†’
Fedha hazijakwamisha maandalizi ya AFCON 2027 - Makonda
Fedha hazijakwamisha maandalizi ya AFCON 2027 - Makonda
50m ago
READ MORE β†’
Fainali CECAFA U20 Kupigwa leo, Tanzania kukutana na Sudan
Fainali CECAFA U20 Kupigwa leo, Tanzania kukutana na Sudan
55m ago
READ MORE β†’
Miss World 2027 kutangaza utamaduni wa Tanzania - Makonda:
Miss World 2027 kutangaza utamaduni wa Tanzania - Makonda:
56m ago
READ MORE β†’
Van Dijk afichua kilichomfanya aendelee na Uholanzi
Van Dijk afichua kilichomfanya aendelee na Uholanzi
2h ago
READ MORE β†’