Ali Kamwe amuomba Samatta arejee Taifa Stars Afcon 2027, Tumuage kama Legend wetu

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
2d ago
Ali Kamwe amuomba Samatta arejee Taifa Stars Afcon 2027, Tumuage kama Legend wetu

Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe, amemuomba Mbwana Samatta kufikiria upya uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa na kurejea kuichezea Taifa Stars katika fainali za AFCON 2027, akisema anastahili kupewa nafasi ya kuaga akiwa uwanjani mbele ya mashabiki.

Kamwe amesema mchango wa Samatta kwa soka la Tanzania unastahili kutambuliwa kwa heshima kubwa, akisisitiza kuwa mchezaji huyo hafai kuishia kuagwa kupitia mitandao ya kijamii.

β€œKwa aliyoyafanya kwenye nchi hii, siyo mchezaji wa kuagwa Instagram,” amesema Kamwe.

Samatta alitangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars Julai 7, 2026, baada ya kuitumikia timu hiyo kwa takribani miaka 15, akisema ulikuwa wakati wa kutoa nafasi kwa kizazi kipya kuendeleza timu ya taifa. Alikuwa nahodha wa Taifa Stars kwa takribani miaka 10 na aliiongoza Tanzania kufuzu AFCON mara tatu.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa mpya kutoka kwa Samatta inayothibitisha kuwa amebadili uamuzi wake kufuatia wito huo. Awali, TFF pia ilisema ingekutana na Samatta na kusikiliza sababu za uamuzi wake, huku wadau wengine wakimtaka aendelee kuitumikia Taifa Stars hadi AFCON 2027.

More Stories

Simba queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
Simba queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
28m ago
READ MORE β†’
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
5h ago
READ MORE β†’
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
7h ago
READ MORE β†’
Kagera sugar yaongeza wazawa benchi la ufundi, Kiemba na Domayo waingia kuungana na Kaze
Kagera sugar yaongeza wazawa benchi la ufundi, Kiemba na Domayo waingia kuungana na Kaze
8h ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda apeleka sakata lake Spata, mazungumzo na Yanga yaanza
Israel Mwenda apeleka sakata lake Spata, mazungumzo na Yanga yaanza
9h ago
READ MORE β†’
Wallace Karia Kukutana na Vilabu vya Ligi Kuu ya Wanawake
Wallace Karia Kukutana na Vilabu vya Ligi Kuu ya Wanawake
12h ago
READ MORE β†’
Fabrice Shema Ajiuzulu Urais wa FERWAFA
Fabrice Shema Ajiuzulu Urais wa FERWAFA
12h ago
READ MORE β†’
Yanga warejea mazoezini, Maandalizi ya mechi zijazo yakianza
Yanga warejea mazoezini, Maandalizi ya mechi zijazo yakianza
1d ago
READ MORE β†’
Manchester city yapinga mashtaka yanayowakabili, ikipanga kuchukua hatua
Manchester city yapinga mashtaka yanayowakabili, ikipanga kuchukua hatua
1d ago
READ MORE β†’
Makonda awaitisha viongozi wa Simba SC.
Makonda awaitisha viongozi wa Simba SC.
1d ago
READ MORE β†’