EXCLUSIVE: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, leo Septemba 29, 2026, ameripotiwa kuwaita viongozi wa Simba SC kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizofikia Xtra90, Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya klabu wanaotokea upande wa MO Dewji, kwa sasa wapo jijini Arusha kwa ajili ya kikao hicho.
Inadaiwa kuwa mazungumzo hayo yanahusu hali ya mambo ndani ya Simba SC, wakati wadau wa klabu hiyo wakisubiri kufahamu kwa undani zaidi ajenda ya kikao pamoja na mambo yatakayojadiliwa na viongozi hao.
Xtra90 itaendelea kufuatilia kinachoendelea Arusha na kukuletea taarifa zaidi pindi zitakapopatikana.