Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, anatarajiwa kukutana na vilabu vya Ligi Kuu ya Wanawake mwanzoni mwa Oktoba 2026, katika jitihada za kutafuta suluhisho la changamoto ya mdhamini wa ligi hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya vilabu, vinavyodaiwa kufikia sita kati ya 12, vilikuwa vikitafakari kususia mashindano kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.
Kikao hicho kinatarajiwa kujadili changamoto zinazovikabili vilabu, huku suala la kupata mdhamini wa ligi likiwa miongoni mwa njia zinazotafutwa ili kuhakikisha mashindano yanaendelea bila vilabu kubeba mzigo mkubwa wa gharama.