Ibrahim Kazimoto avutia benchi la Yanga, hatua mpya yaibua kitu kikubwa

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
1h ago
Ibrahim Kazimoto avutia benchi la Yanga, hatua mpya yaibua kitu kikubwa

Kinda wa Yanga SC, Ibrahim Kazimoto, ameanza kuonyesha dalili za kuwa moja ya vipaji vinavyoweza kuwa na nafasi kubwa ndani ya kikosi cha kwanza, baada ya kiwango chake kuwavutia makocha wa timu hiyo.

Kocha wa timu za vijana za Yanga, Mohamed Badru, amesema kocha wa kikosi cha kwanza, Manqoba Mngqithi, amevutiwa na uwezo wa Kazimoto tangu alipopandishwa kutoka timu ya U-20.

Badru amesema Kazimoto ana baadhi ya sifa zinazohitajika katika soka la kisasa, ikiwemo nguvu, kasi, uwezo wa kupambana na uelewa wa kiufundi, jambo lililompa nafasi ya kuanza kuonekana katika kikosi cha kwanza. Kwa Badru, kupandishwa kwa Kazimoto si jambo la bahati.

Kocha huyo amesema ilikuwa sehemu ya mpango wake tangu alipoanza kufanya kazi Yanga, akilenga kuona angalau mchezaji mmoja au wawili kutoka U-20 wakipenya kikosi cha kwanza msimu huu.

Hata hivyo, Badru anaonya kuwa safari ya Kazimoto bado ndiyo inaanza. Anahitaji kuendelea kufanyiwa kazi kiufundi, kuvumilia ushindani na kujifunza kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu ili kufikia kiwango cha juu zaidi.

More Stories

Siku 260 kuelekea Afcon 2027, Afrika mashariki ikiibeba Afrika mzima
Siku 260 kuelekea Afcon 2027, Afrika mashariki ikiibeba Afrika mzima
49m ago
READ MORE β†’
Steve Barker na siri ya mpango wa Simba kuelekea Derby ya Kariakoo
Steve Barker na siri ya mpango wa Simba kuelekea Derby ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simbu kunogesha Simba marathon 2026, Coco beach kuwaka moto
Simbu kunogesha Simba marathon 2026, Coco beach kuwaka moto
1h ago
READ MORE β†’
Kibadeni na historia ya Hat-Trick ya Kariakoo Derby
Kibadeni na historia ya Hat-Trick ya Kariakoo Derby
3h ago
READ MORE β†’
Bernard Kamungo akamilisha taratibu za kuichezea Taifa Stars.
Bernard Kamungo akamilisha taratibu za kuichezea Taifa Stars.
13h ago
READ MORE β†’
Ronaldo Aondoka, wafuasi milioni 8 zapotea Ureno, nini kinaendelea nyuma ya pazia?
Ronaldo Aondoka, wafuasi milioni 8 zapotea Ureno, nini kinaendelea nyuma ya pazia?
22h ago
READ MORE β†’
Ghana yamfuta kazi Queiroz baada ya kufungwa mechi mbili kufuzu Afcon 2027
Ghana yamfuta kazi Queiroz baada ya kufungwa mechi mbili kufuzu Afcon 2027
22h ago
READ MORE β†’
Takwimu za kiungo wa boli Duke Abuya akiingia Derby ya Kariakoo Oktoba 10
Takwimu za kiungo wa boli Duke Abuya akiingia Derby ya Kariakoo Oktoba 10
23h ago
READ MORE β†’
Simba kujipima na Timu za Afrika kusini, ikijiandaa na muendelezo wa msimu 2026-27
Simba kujipima na Timu za Afrika kusini, ikijiandaa na muendelezo wa msimu 2026-27
23h ago
READ MORE β†’
Messi kupewa shahada ya juu ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
Messi kupewa shahada ya juu ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
1d ago
READ MORE β†’