Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, amesema maandalizi ya Kariakoo Derby ya Oktoba 10 yamehusisha hatua mpya za kiusalama, ikiwemo matumizi ya kifaa maalum cha kugundua harufu katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Cornel amesema kifaa hicho kitatumika katika mchezo wa Simba dhidi ya Yanga, utakaochezwa Oktoba 10, ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa kuhakikisha mazingira ya mchezo yanakuwa salama na yanazingatia taratibu zinazotakiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TFF jijini Dar es Salaam, Cornel amesema kifaa hicho hakitatumika kwenye Kariakoo Derby pekee, bali kitaendelea kutumika pia katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hatua hiyo inaongeza teknolojia mpya katika usimamizi wa mazingira ya michezo, huku macho yote yakielekezwa kwenye Kariakoo Derby ya Oktoba 10 ambayo tayari imeanza kuleta maandalizi ya aina yake.