Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, amesema makocha wa Simba na Yanga watapewa kadi mbili katika Kariakoo Derby ya Oktoba 10, ambazo zitatumika kuomba review ya matukio kupitia mfumo wa FIFA Video Support (FVS).
Cornel amesema utaratibu huo ni sehemu ya hatua mpya za matumizi ya teknolojia katika kusimamia mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, huku makocha wakipewa nafasi ya kuomba mapitio ya matukio wanayoona yanahitaji kuchunguzwa zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TFF jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo, Cornel amesema mfumo huo hautatumika kwenye Kariakoo Derby pekee, bali kadi hizo zitatumika pia katika michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kariakoo Derby ya Oktoba 10 inatarajiwa kuwa moja ya mechi zitakazoweka matumizi ya mfumo huo katika uangalizi mkubwa, huku Simba na Yanga zikijiandaa kukutana katika mchezo unaobeba presha kubwa ndani na nje ya uwanja.