Ufaransa imefanya comeback kubwa na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, baada ya kuanza mchezo ikiwa nyuma kwa bao 1-0. Mabadiliko makubwa yalikuja baada ya kuingia kwa kiungo mshambuliaji Michael Olise, ambaye alibadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo.
Olise aliingia uwanjani dakika ya 60, na ndani ya muda mfupi akaonyesha ubora wake kwa kuhusika moja kwa moja kwenye mabao matatu. Nyota huyo alifunga mabao mawili na kutoa assist moja ndani ya dakika 25, akiiongoza Ufaransa kurejea mchezoni na kugeuza matokeo.
Kwa kiwango hicho, Olise ameendelea kuonyesha kwa nini amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaovutia zaidi kwa sasa. Kasi, ubunifu na uwezo wake wa kutengeneza nafasi vilifanya Ufaransa ionekane kama timu tofauti kabisa baada ya kuingia kwake.
Kwa msimu huu, Olise ameripotiwa kuwa na jumla ya mabao 12 na assists 5 katika mechi 11, akifikisha jumla ya goal contributions 17 akiwa na klabu na timu ya taifa. Takwimu hizo zinaonyesha kiwango cha juu ambacho nyota huyo wa Ufaransa anaendelea kukifikia.
Olise amewasha moto, na safari hii Ufaransa imepata ushindi wa 4-1 baada ya kugeuza mchezo uliokuwa umeanza kwa presha.