Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Ahmad Ally, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate, huku akitambua uzoefu na ubora wa mbinu wa kocha wa wapinzani wao, Fred Felix.
Mchezaji wa JKT Tanzania, Offen Chikola, amesema wachezaji wamepokea maelekezo ya kutosha kutoka kwa kocha na jukumu lao sasa ni kwenda kuyatekeleza uwanjani.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa Fountain Gate, Fred Felix βMinziroβ, amesema mapumziko waliyopata yamewapa nafasi ya kufanya marekebisho katika kikosi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania, huku akitambua ubora wa wapinzani wao.
Naye mchezaji wa Fountain Gate, Derick Mukombozi, amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo, akisema maandalizi waliyofanya yamewaweka tayari kwa mchezo huo.