Joto la Kariakoo Derby linazidi kupanda, huku wanawake mashabiki wa Simba maarufu kama “Gwede Gwede” wakitoa tambo zao usiku huu kuelekea mchezo huo dhidi ya Yanga.
Wanawake hao waliovalia sare za khanga za timu yao wamewataka Msemaji wa Simba, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuondoa hofu na kuwa na imani na timu yao, wakisisitiza kuwa safari hii wanaamini ushindi utatua upande wa Msimbazi.
Wamesema “unyonge” wa Simba dhidi ya Yanga umefika mwisho, huku wakiahidi kuzunguka tawi kwa tawi kuhamasisha mashabiki na kuhakikisha hamasa kuelekea mchezo huo inakuwa kubwa.
Mmoja wa wanachama wa kundi hilo, Suzan Mrassy, amesema yuko tayari kutoa zawadi mbalimbali kwa wachezaji kama sehemu ya kuwapa motisha kuelekea Kariakoo Derby.
Kauli hizo zimeongeza joto la dabi nje ya uwanja, huku tambo kutoka kwa mashabiki wa pande zote mbili zikizidi kushika kasi kadri Oktoba 10 inavyokaribia.