Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
1h ago
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.

Simba SC imeendeleza makali yake katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania baada ya kuichapa Mashujaa FC mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Libasse Gueye alianza kuifungia Simba dakika ya 16, kabla ya Elie Mpanzu kuongeza bao la pili dakika ya 33. Hata hivyo, Mashujaa ilikumbwa na pigo kubwa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza baada ya Hassan Kabunda kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45+6.

Kipindi cha pili Simba iliendelea kutawala mchezo huo. Anicet Oura alifunga bao la tatu dakika ya 53, kabla ya Mpanzu kuongeza bao lake la pili na la nne kwa Simba dakika ya 58. Morice Abraham aliendeleza karamu ya mabao dakika ya 61.

Mashujaa ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Seleman Bwenzi dakika ya 64, akifunga kwa shuti kali la kiwango cha juu. Hata hivyo, Ismail Touré aliihakikishia Simba ushindi mnono kwa kufunga bao la sita dakika ya 68.

Matokeo ya mwisho: Simba SC 6-1 Mashujaa FC.

ADVERTISE HERE

More Stories

Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
2h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
10h ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
10h ago
READ MORE β†’
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
11h ago
READ MORE β†’
Mechi zote za 15 de Agosto na Simba SC kuchezwa Dar es Salaam
Mechi zote za 15 de Agosto na Simba SC kuchezwa Dar es Salaam
12h ago
READ MORE β†’
Ligi ya mabingwa Ulaya: United, Barca, Arsenal, Bayern mzigoni leo
Ligi ya mabingwa Ulaya: United, Barca, Arsenal, Bayern mzigoni leo
12h ago
READ MORE β†’
Simba kurejea uwanjani leo kuivaa Mashujaa NBC Premier League.
Simba kurejea uwanjani leo kuivaa Mashujaa NBC Premier League.
13h ago
READ MORE β†’
Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
1d ago
READ MORE β†’
Simba SC yaendeleza ubabe, yabaki bila kipigo baada ya mechi saba
Simba SC yaendeleza ubabe, yabaki bila kipigo baada ya mechi saba
1d ago
READ MORE β†’