Tanzania imeendelea kuandika historia katika soka la kimataifa baada ya klabu za Azam FC na Singida Black Stars kufanikiwa kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) kwa msimu wa 2026/27.
Hatua hiyo inafanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye uwakilishi mkubwa zaidi msimu huu, ikijumuisha pia miamba ya soka Yanga na Simba SC zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL).
Azam FC na Singida Black Stars zimeingia hatua hiyo kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuonyesha viwango safi na kupita kigingi cha raundi ya pili ya mchujo dhidi ya wapinzani wao.
Hatua hiyo ya makundi ambayo droo yake itafanyika Jumatano Oktoba 28, inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kufuatia kuwepo kwa vigogo wengine wa soka la Afrika waliofuzu.
Kati ya timu zilizofuzu ni pamoja na Al Ahly SC ya Misri, USM Alger ya Algeria (waliofuzu kufuatia wapinzani wao kujiondoa), na Raja Casablanca kutoka Morocco.
Orodha kamili ya timu zilizofuzu hatua ya makundi inajumuisha:
- Tanzania: Azam FC, Singida Black Stars
- Misri: Al Ahly SC
- Algeria: USM Alger
- Morocco: Raja Casablanca
- Tunisia: CS Sfaxien
- Libya: Al Ahli Tripoli
- Angola: 1º de Agosto
- Zambia: Red Arrows
- Mozambique: Black Bulls
- Mali: Real Bamako
- DRC: AS Maniema Union
- Afrika Kusini: Durban City FC
- Togo: ASKO Kara