Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesisitiza umuhimu wa wachezaji wake kucheza kwa moyo, huku wakitumia akili na ujanja wa kisoka wanapokabiliana na wapinzani wao.
Ibenge ameeleza kuwa wachezaji wanapaswa kuwa makini na kubadilika kulingana na mwenendo wa mchezo, akibainisha kuwa wapinzani wanaweza kubadili mbinu zao wakati wowote ndani ya dakika 90.
<>Kauli hiyo ya kocha huyo imekuja kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City, unaotarajiwa kuchezwa kesho, huku Azam FC ikijiandaa kukabiliana na changamoto ya wapinzani wake.
ADVERTISE HERE