Kocha wa Mbeya City, Salim Mayanga, amesema kikosi chake kimetumia muda uliopatikana kufanyia kazi mapungufu na kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita.
Mayanga ameeleza kuwa maandalizi hayo yanalenga kukiweka kikosi chake katika hali nzuri kabla ya kukutana na Azam FC, huku wakitambua ubora wa wapinzani wao katika nyanja za kiufundi na kimbinu.
Kauli hiyo imekuja kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Azam FC na Mbeya City, unaotarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 28, huku Mbeya City ikilenga kuonyesha ushindani baada ya kufanya marekebisho katika maeneo yaliyokuwa na mapungufu.
ADVERTISE HERE