Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo uliotangazwa hivi karibuni ni batili na haramu, kauli inayoongeza uzito wa mjadala kuhusu mustakabali wa uongozi wa wekundu hao wa Msimbazi.
Mangungu amesema kuwa kwa sasa kama uongozi wapo kwenye mazungumzo na serikali kuona namna gani wanalienda swala la mabadiliko ndani ya timu hiyo na hawapo tayari kwa namna yeyote kuona wanatingishwa katika swala ilo.
"Mchakato huu ambao umetangazwa ni mchakato batili na haramu, tupo kwenye mashauliano na serikali kuona namna bora kuliendea ili jambo linalohusu mabadiliko na uwekezaji ili ufikie mwisho, sasa hatutaki watu watutingishe apa katikati" amesema Mangungu.
Mangungu amesema hayo hii leo kwenye mkutano wa wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es salaam