TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1h ago
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kusimamia moja kwa moja mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba SC baada ya kubaini mapungufu katika ratiba na utaratibu wa uchaguzi uliotangazwa awali na klabu hiyo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia Katiba ya Simba SC, kanuni za uchaguzi pamoja na taratibu zinazotakiwa kisheria.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kiburu Kibamba, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati kupokea malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company katika kuandaa mchakato huo.

Kibamba amesema kamati ilipokea barua mbili kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF. Barua ya kwanza ilihusu taarifa ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa Simba SC, huku ya pili ikiwa na malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na bodi hiyo.

Kutokana na malalamiko hayo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaita na kuwasikiliza wahusika wa pande zote mbili kabla ya kutoa maelekezo kuhusu hatua zinazopaswa kufuatwa katika kuendeleza mchakato huo.

Katika mazungumzo hayo, kamati ilikutana na wawakilishi wa pande mbili zinazohusika, akiwamo Crescentius Magori aliyewakilisha upande wa mwekezaji na Murtaza Mangungu aliyewakilisha upande wa wanachama.

Kibamba amefafanua kuwa baada ya kupitia utaratibu uliotangazwa awali, kamati imebaini mapungufu katika ratiba ya uchaguzi, hivyo imeamua kuiboresha kabla ya kutangaza ratiba mpya itakayoongoza mchakato kuelekea uchaguzi huo.

Hatua hiyo ya TFF inatarajiwa kuweka utaratibu wa uchaguzi katika mfumo unaozingatia kanuni na taratibu husika, huku wadau wa Simba SC wakisubiri ratiba iliyoboreshwa na maelekezo zaidi kuhusu hatua zinazofuata.

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
4h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
4h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
4h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
7h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
19h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
21h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
21h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
22h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
23h ago
READ MORE β†’