Inter Miami imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya New England Revolution katika mchezo wa MLS, huku Lionel Messi akiwa mhimili mkuu wa ushindi huo baada ya kuchangia mabao mawili (2 G/A).
Messi alionyesha ubora wake kwa kufunga bao na kutoa asisti iliyosaidia Inter Miami kubadili matokeo na kuondoka na ushindi muhimu wa ugenini.
Nyota huyo wa Argentina ameendelea kuwa mwiba kwa New England Revolution, akiwa amehusika moja kwa moja katika mabao 14 katika michezo sita dhidi ya timu hiyo, akifunga mabao nane na kutoa asisti sita.
Kwa wastani, Messi amechangia wastani wa 2.3 ya mabao katika mchezo dhidi ya New England Revolution.
Mbali na kuiongoza Inter Miami kwenye ushindi huo, matokeo hayo yameisaidia timu hiyo kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Messi pia ameendelea kuongeza takwimu zake za kihistoria, akiwa amefikisha asisti 428 na mabao 937 katika maisha yake ya soka.
Lionel Messi, ubora unaoendelea kuandika historia.