Simba SC imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa NBC Premier League uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kurejea mchezoni kufuatia kuwa nyuma kwa mabao 2-1.
Anicet Oura aliipa Simba bao la mapema dakika ya 4, lakini Raymond Lulendi aliibadilishia Namungo matokeo kwa kufunga mabao mawili dakika ya 36 na 43, na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili Simba ilirejea kwa nguvu kusaka matokeo, huku beki Rushine De Reuck akisawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 80 na kuamsha matumaini ya mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi.
Dakika ya 89, Anicet Oura alifunga bao lake la pili katika mchezo huo na kukamilisha comeback ya Simba, ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Pongezi pia kwa Ibrahim Doumbia, ambaye aliingia akitokea benchi na kuathiri mchezo moja kwa moja baada ya kusababisha penalti iliyoisaidia Simba kurejea mchezoni.
Simba SC yaonyesha tabia ya kupambana hadi dakika za mwisho na kuondoka na pointi tatu muhimu.